Serikali Yaongeza Mishahara Kwa Watumishi wa Umma 35.1%

Filed in Forum by on May 1, 2025 0 Comments

Singida, Mei 1, 2025 – Katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Singida, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza nyongeza ya kima cha chini cha mshahara kwa Watumishi wa Umma kwa asilimia 35.1 kuanzia mwezi Julai 2025.

 Mishahara Kwa Watumishi wa Umma 35.1%

Mishahara Kwa Watumishi wa Umma 35.1%

Rais Samia alisema nyongeza hii ni sehemu ya juhudi za Serikali katika kuthamini mchango mkubwa wa wafanyakazi waliokubali kubana matumizi kipindi cha changamoto za kiuchumi na kuendelea kufanya kazi kwa bidii, hali iliyopelekea uchumi wa nchi kukua kwa asilimia 5 mwaka huu.

“Mcheza kwao hutunzwa, na kwa kuwa uchumi umekua kwa sababu ya juhudi zenu, ninayo furaha kutangaza ongezeko hili,” alisema Rais Samia.

Kwa mujibu wa Rais Samia, kima cha chini cha mshahara kitaongezeka kutoka TSh. 370,000 hadi TSh. 500,000, huku ngazi nyingine za mishahara pia zikitarajiwa kuongezeka kulingana na bajeti ya Serikali.

Mabadiliko ya Kima cha Chini cha Mshahara kwa Watumishi wa Umma

Kipengele Kabla ya Ongezeko Baada ya Ongezeko (Julai 2025) Asilimia ya Ongezeko
Kima cha Chini cha Mshahara TSh. 370,000 TSh. 500,000 35.1%

Kauli ya Rais Samia:

“Mwaka jana tuliwasihi wafanyakazi kuvumilia kutokana na hali ya uchumi. Lakini sasa kwa mapenzi makubwa na kutokana na mshikamano wenu, Serikali imeamua kuongeza mishahara. Nyongeza hii ni ishara ya kuthamini juhudi zenu.”

Serikali pia imeahidi kwamba nyongeza za mishahara kwa ngazi nyingine zitazingatia uwezo wa bajeti, huku ikiendelea kutoa maslahi na motisha kwa watumishi wa umma.

Soma Zaidi:

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *