Tangazo la ajira JWTZ 2025 Nafasi Za Kujiunga Jeshini

Filed in Fursa Za Ajira, Nafasi za Kazi by on May 1, 2025 0 Comments

Hili ni Tangazo la ajira JWTZ 2025 Nafasi Za Kujiunga Jeshini, pia tumekuandalia makala hii ya Nafasi za kazi jwtz 2025 kwene pdf download.

TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatangaza nafasi za kuandikishwa jeshini kwa vijana wa Kitanzania wenye elimu kuanzia Sekondari hadi elimu ya juu. Uandikishaji huu pia utahusisha vijana wenye taaluma adimu.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)

Wataalamu watakaoandikishwa jeshini watapatiwa mafunzo mbalimbali ya kijeshi pamoja na mafunzo ya kuwaendeleza kitaaluma.

SIFA ZA MWOMBAJI

Mwombaji anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:

  • Awe raia wa Tanzania mwenye kitambulisho cha Taifa.
  • Awe na afya njema na akili timamu.
  • Awe na nidhamu, asiwe amewahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai.
  • Awe na cheti halisi cha kuzaliwa, vyeti vya shule na taaluma.
  • Awe hajatumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au KMKM.
  • Awe amehitimu mafunzo ya JKT kwa mkataba wa kujitolea au mujibu wa sheria.
  • Umri:
    • Kidato cha Nne/Sita: miaka isiyozidi 24
    • Stashahada: miaka isiyozidi 26
    • Elimu ya Juu: miaka isiyozidi 27
    • Madaktari Bingwa: miaka isiyozidi 35

TAALUMA ADIMU ZINAZOHITAJIKA

Kundi la Taaluma Maelezo ya Taaluma
Tiba – Medical Doctor (Specialist): General Surgeon, Orthopaedic Surgeon, Urologist, Radiologist, ENT Specialist, Anaesthesiologist, Physician, Ophthalmologist, Paediatrician, Obstetrician & Gynaecologist, Oncologist, Pathologist, Psychiatrist, Emergency Medicine Specialist, Haematologist.
– Medical Doctor, Dental Doctor, Veterinary Medicine, Bio Medical Engineer, Dental Lab Technician, Anaesthetic, Radiographer, Optometry, Physiotherapy, Aviation Doctor.
Uhandisi Bachelor of Electronic Engineering, Mechanical Engineering, Marine Engineering, Marine Transportation and Nautical Science, Mechanics in Marine Diesel Engine, Aviation Management, Aircraft Accident and Incident Investigation, Meteorology, Air Traffic Management, Aeronautic Engineering.
Fundi Mchundo Aluminium Welding, Welding and Metal Fabrication.

UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI

Maombi yote yaandikwe kwa mkono na yawasilishwe Makao Makuu ya Jeshi, Dodoma kuanzia tarehe 01 Mei, 2025 hadi 14 Mei, 2025.

Viambatisho vinavyotakiwa:

  • Nakala ya Kitambulisho cha Taifa au Nambari ya NIDA
  • Nakala ya cheti cha kuzaliwa, vyeti vya shule na chuo
  • Nakala ya cheti cha JKT (kwa waliomaliza mkataba wa kujitolea)
  • Nambari ya simu ya mkononi ya mwombaji

Jinsi Ya Kutuma Maombi Ya Ajira za JWTZ

Mkuu wa Utumishi Jeshini
Makao Makuu ya Jeshi
Sanduku la Posta 194
DODOMA, TANZANIA

Kwa Taarifa Zaidi: https://www.tpdf.mil.tz/

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *