TANGAZO LA KUITWA KAZINI WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA (TFS) NA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI (TAWA) 30-04-2025
TANGAZO LA KUITWA KAZINI WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA (TFS) NA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI (TAWA) 30-04-2025, Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 06-03-2025 na tarehe 28-03-2025 kuwa matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyo orodheshwa katika tangazo hili.

KUITWA KAZINI WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA
Orodha ya majina haya pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.
Wasailiwa wote waliofaulu usaili na kupangiwa vituo vya kazi, BARUA zao za kupangiwa vituo vya kazi watazipata kupitia AKAUNTI zao za Ajira Portal kwenye sehemu ya My Applications, hivyo watapaswa kupakua na kutoa nakala (Download and Print) barua hizo na Kwenda nazo kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa.
Aidha, waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa kituo cha kazi wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri katika muda ambao umeainishwa kwenye barua za kupangiwa kituo cha kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) za masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya Ajira.
Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.