TANGAZO LA NAFASI YA KAZI HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE 29-04-2025
TANGAZO LA NAFASI YA KAZI HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE 29-04-2025, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Manispaa ya Temeke kuomba nafasi ya kazi iliyotajwa hapo chini, baada ya kupokea kibali chenye Kumb. Na. FA. 228/613/01F/100 cha tarehe 13 Machi, 2025 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

NAFASI YA KAZI HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE
1. DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 01
- MAJUKUMU YA KAZI YA DEREVA II
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari
- Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari
- Kutunza na kuandika daftari la safari “log book” kwa safari zote
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali,
- Kufanya usafi wa Gari
- Kufanya kazi nyigine kadri atakavyoelekezwa na msimamizi
1.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu Kidato cha Nne (IV) na kupata Cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV). Awe na leseni daraja ‘C’ au ‘E’ ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali, Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji Magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha Mafunzo ya ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
1.1.3 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali TGS – B
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45;
- Waomabji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuaninisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya ulemavu walionao.
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/ Wakili;
- Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa zakuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
- Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/ Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Testmonials Provisional Results Statement of Rusults hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji walisoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE)
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji watakao wasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za
- Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 12 Mei, 2025
- Muhimu: Kumbuka Kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamaoja na vyeti vya elimu.Barua zote za maombi ziandikwe kwa;
MKURUGENZI WA MANISPAA, HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE,
- L. P 46343, DAR ES SALAM.
- Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal kupitia anuani ifuatayo: https://portal.ajira.go.tz Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘ “Recruitment Portal’
xiv. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATASHUGHULIWA.
Makala Nyingine: