Majina Ya Walioitwa kwenye mafunzo ya jeshi la Zimamoto na Uokoaji 2025

Filed in Usaili by on May 3, 2025 0 Comments

Majina Ya Walioitwa kwenye mafunzo ya jeshi la Zimamoto na Uokoaji 2025 (Usaili Jeshi la Zimamoto).  JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linapenda kuwatangazia waombaji wote walioteuliwa kuwa wamechaguliwa kuhudhuria mafunzo ya Uaskari ngazi ya Konstebo. Mafunzo haya yatafanyika katika Chuo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilichopo Chogo, Wilaya ya Handeni, Mkoa wa Tanga.

Walioitwa kwenye mafunzo ya jeshi la Zimamoto

Walioitwa kwenye mafunzo ya jeshi la Zimamoto

TAREHE YA KUFIKA CHUONI

Wahusika wote wanatakiwa kufika chuoni kuanzia tarehe 16 Mei, 2025 hadi tarehe 18 Mei, 2025 bila kukosa.
Angalizo: Mtu yeyote atakayeshindwa kufika ndani ya tarehe hizi hatapokelewa chuoni, na nafasi yake itapewa mtu mwingine.

MAELEKEZO YA SAFARI

Fika katika Kituo cha Kabuku, ambacho kiko kilomita 12 kutoka chuoni.
Chuo kimeandaa utaratibu maalumu wa kuwapokea wahusika kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 4:00 usiku kwa tarehe zilizotajwa.

GHARAMA BINAFSI

Mhusika atagharamia:

  • Nauli ya kwenda chuoni
  • Chakula na malazi kwa siku zote ambazo hajapokelewa rasmi

VYETI MUHIMU KUVILETA

Mhusika anatakiwa kufika na:

  1. Vyeti halisi vya masomo, taaluma au ujuzi alioombea
  2. Cheti cha kuzaliwa
  3. Kitambulisho cha NIDA au namba ya NIDA
  4. Leseni halali ya udereva (kwa walioomba nafasi ya udereva)
  5. Nakala tatu (03) kwa kila cheti

Angalizo: Majina yaliyomo katika vyeti vyote lazima yafanane. Mhusika ambaye majina yake yatatofautiana hatapokelewa na nafasi yake itachukuliwa na mtu mwingine.

VIPIMO VYA AFYA

Mhusika atapimwa:

  • Afya ya mwili
  • Afya ya akili
  • Mimba (kwa wanawake)

Atakayebainika kuwa na kasoro za kiafya hataruhusiwa kuendelea na mafunzo, na atarudishwa kwa gharama zake mwenyewe.

VIFAA VYA LAZIMA KUVILETA

  1. Mashuka 2 ya rangi ya bluu
  2. Mto 1
  3. Foronya 2 za rangi ya bluu
  4. Chandarua 1 (rangi ya bluu, duara)
  5. Ndoo ya plastiki ya lita 20
  6. Sahani ya bati
  7. Kikombe cha bati
  8. Fedha kwa matumizi binafsi
  9. Bima ya afya (kwa waliyonayo)

VIFAA VITAKAVYONUNULIWA CHUONI

  • Raba za michezo
  • Fulana (T-shirt) ya bluu
  • Madaftari makubwa (counter books 4 quire – pcs 5)
  • Vifaa vya michezo (tracksuit, bukta bluu, fulana)
  • Kalamu

ORODHA YA WALIOCHAGULIWA

KUITWA KWENYE MAFUNZO JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI CHUONI CHOGO

Tafadhali angalia orodha kamili ya majina ya waliochaguliwa katika mafunzo haya kwenye kiambatisho au tovuti rasmi ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na ofisi ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Imetolewa na:
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Mei, 2025

Makala Nyingine:

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *